SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR YAAZIMIA USHIRIKI WA KISHINDO MAONESHO YA EXPO 2025 OSAKA JAPAN
- April 22, 2025

19, APRILI 2025.
Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara Dkt Hashil T. Abdallah na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Dr. Said S. Mzee wameshiriki kikao kazi cha Makatibu Wakuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Wadau wa Sekta binafsi na kuongea na waandishi wa habari ambapo kwa pamoja wameazimia kuwa na ushiriki wa kishindo katika maonesho ya Biashara ya Dunia EXPO 2025 OSAKA, JAPAN.
Kupitia maonesho hayo ya Dunia Watanzania watapata fursa ya kukutana na wadau mbalimbali kutoka nchi zaidi ya 160 katika sekta za Utalii, Miundombinu, Sanaa, Sayansi na Teknolojia, Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Uchumi wa Buluu, Afya, Lugha ya Kiswahili na Utamaduni, Nishati, na Uwekezaji." ameeleza Dr. Hashil.