Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

Majukumu


1. Kukuza na Kuendeleza Biashara
• Kuandaa maonesho ya biashara ya kitaifa na kimataifa (mfano: Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam – Sabasaba).
• Kutangaza bidhaa za Tanzania katika masoko ya nje.
• Kuwezesha wafanyabiashara wa Tanzania kushiriki maonesho ya kimataifa.

2. Utafiti na Taarifa za Masoko
• Kukusanya na kusambaza taarifa za masoko ya ndani na nje.
• Kutoa ushauri wa kibiashara kwa wauzaji na wazalishaji.
• Kuchapisha takwimu na ripoti za biashara.

3. Uwezeshaji wa Mauzo ya Nje
• Kusaidia wauzaji wa Tanzania kupata masoko mapya.
• Kutoa mafunzo kuhusu taratibu za usafirishaji, viwango na vyeti.
• Kusaidia biashara kufuata masharti ya kimataifa ya biashara.

4. Utekelezaji wa Sera
• Kushauri serikali kuhusu sera na mikakati ya biashara.
• Kutekeleza mipango ya kitaifa ya maendeleo ya biashara.
• Kushirikiana na wizara, sekta binafsi na mashirika ya kimataifa.

5. Kujenga Uwezo
• Kutoa mafunzo kwa wajasiriamali na SMEs ili kuongeza ushindani.
• Kuwezesha wanawake na vijana kushiriki kikamilifu katika biashara.
• Kufundisha kuhusu ubora wa bidhaa, ufungashaji na uuzaji.