SABASABA MWAKA HUU 2024 KUWA WA KIPEKEE
- June 21, 2024

20/6/2024
Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania Bi Latifa M.
Khamis ameeleza kuwa maandalizi ya Maonesho 48 ya Biashara ya Kimataida ya Dar
es Salaam (Sabasaba) yatakayoanza tarehe 28 Juni, hadi tarehe 13 Julai, 2024 kuwa
yanaendelea vizuri na kubainisha kuwa mwaka huu 2024 yatakuwa ya kipee wakati
akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Bi Latifa ameeleza kuwa maonesho haya yameboreshwa ikiwa ni pamoja na wananchi
kuweza kukata tiketi kupitia mitandao ya simu ambapo Tantrade imeshirikiana na
mtandao wa Vodacom hivyo wananchi wataweza kukata tiketi zao, hata hivyo bado
utaratibu wa kukata tiketi mlangoni utakuwepo kwa ajili ya wachache ambao
watashindwa kukata mtandoni.
Vilevile Mkurugenzi Latifa ameendelea kueleza kuwa maombi ya vitambulisho
yameanza na yanaendelea kupitia mitandao ambao ofisi inaendelea kutangaza (trade
fair.tantrade. go.tz) ikiwa ni pamoja na matumizi ya mageti ya kieletroniki ambapo
wananchi na magari yatatumia kuingia, mfumo huu utapunguza usumbufu wa foleni
pamoja na watu kuweza kuingia ndani kwa urahisi,
Aidha amesema kuwa hadi sasa nchi 25 zimeshakwisha kuthibitisha ushiriki wake
katika maonesho haya na kueleza kuwa hizi ni jitihada za Rais wa Jamuhuri wa
Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwa anaitangaza
Tanzania nje ya nchi, kupitia nchi hizi Maonesho haya yamepata makampuni ya nje
ambapo Mdhamini Mkuu wa maonesho haya ambaye ni East Africa Commercial and
Logistic Centre anatarajia kuleta makampuni zaidi ya 300 kutoka nchini China , pamoja
na ushiriki wa majimbo zaidi ya 9 yaliyopewa udhamini nusu na serikali yao , ikifuatiwa
na nchi ya Misri yenye makampuni 35 pamoja na nchi nyingine, ambazo zitakua na
programu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusheherekea siku za mataifa saba (7)
(National days) na siku za mashirika (cooperate days ) ambazo zitaongeza uhusiano
na fursa za kibiashara kwa wafanyabiashara.
Bi Latifa ameendelea kueleza kuwa maonesho haya yatakua na makampuni ya ndani
ya nchi 2979 ambayo yanajumuisha, makampuni binafsi, wizara, na taasisi za serikali,
pamoja na kampuni 223 za nje ya nchi. Maonesho haya yataleta ustawi na maendeleo
ya jamii kwa kuongeza ajira kwa mtu mmoja mmoja, ajira za jamii kwa wale wanaofanya
biashara za huduma za kijamii kama wauzaji wa vyakula, sekta ya usafirishaji, pamoja
na hoteli ambazo zinawapokea wageni kutoka ndani na nje ya nchi, pamoja na kulipa
kodi kwa nchi ambapo ni chachu katika ukuaji wa Uchumi wa nchi yetu.