Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

KONGAMANO LA BIASHARA LA TANZANIA NA IRAN LAFUNGULIWA RASMI.

  • October 17, 2024

16, Oktoba 2024.

 Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Saidi Jafo  amefungua rasmi kongamano la biashara baina ya Tanzania na  nchi ya Iran, ambapo ni siku ya kwanza ya kongamano hilo litakalofanyika kwa siku nne kuanzia leo tarehe 16  hadi 19 Oktoba 2024 likihusisha Viongozi, wafanyabiashara na wadau  wa sekta mbalimbali  ikiwa ni pamoja Kilimo, Ufugaji,  Ujenzi, Madini na nyinginezo wakijadili namna ya kushirikiana katika kubadilishana na kutumia fursa zilizopo pande zote mbili na kuchochea ukuaji wa  uchumi kwa nchi hizi.
Kongamano hili la Biashara baina ya Tanzania na Iran limeratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) na linafanyika katika Ukumbi wa Kilimanjaro uliopo Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere maarufu kama (Sabasaba), Kilwa Road Dar es Salaam.