MKUTANO WA MAENDELEO YA UCHUMI BAINA YA TANZANIA NA MAREKANI WAZAA MATUNDA
- March 12, 2025

11 Machi 2025
Dar es Salaam.
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)imeratibu na kushiriki Mkutano wa Maendeleo ya Uchumi baina ya Tanzania na Marekani kwa lengo la kuangazia Mikakati mbalimbali ya Kimaendeleo katika Sekta ya Uchumi na kuweka mazingira rafiki ya Uwekezaji kwenye Biashara, Viwanda na Kilimo. Mkutano huo umefanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini, Dar es Salaam.
Aidha Mkurugenzi wa Usimamizi wa Biashara Bi. Lulu Mkudde ametumia fursa hiyo kubainisha fursa za biashara zilizopo Tanzania na kuwakaribisha wadau wa maendeleo ya Uchumi kutoka Marekani kutumia fursa hizo kwa maendeleo ya nchi zote mbili. Kadhalika, Bi. Lulu amewakaribisha kushiriki Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam 2025, yatakayofanyika kuanzia tarehe 28 Juni hadi tarehe 13 Julai, 2025.