TANZANIA KUTENGENEZA MAZINGIRA RAFIKI YA BIASHARA KWA WAFANYABIASHARA WA DUBAI
- December 12, 2024

12/12/2024
Dar es salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Selemani Jafo ameshiriki kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Umoja wa nchi za Falme za Kiarabu (UAE) ambalo limeratibiwa na TanTrade, TIC, TCCIA na Chemba ya Dubai huku likihudhuriwa na taasisi mbalimbali pamoja na wafanyabiashara 391 kutoka Tanzania na ujumbe kutoka nchi ya Dubai kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa Johari Rotana Jijini Dar es salaam leo tarehe 12 Desemba, 2024.
Mhe. Waziri Jafo amesema kuwa serikali ya Tanzania inatengeneza mazingira rafiki pamoja na kupunguza vizuizi mbalimbali vya kibiashara kwa wafanyabiashara mbalimbali kutoka nchi za kigeni ikiwa ni pamoja na nchi kutoka Falme za Kiarabu.