KONGAMANO LA UWEKEZAJI NA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA MISRI
- May 7, 2026
KONGAMANO LA UWEKEZAJI
NA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA MISRI
Fursa za Kizazi Kipya”
Kongamano hili ni
jukwaa la kipekee linalowakutanisha wadau wa sekta mbalimbali kutoka Tanzania
na Misri kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara. Kupitia
tukio hili, washiriki watapata nafasi ya:
- Kujenga mitandao ya kimataifa na
wawekezaji, wafanyabiashara, na taasisi za kifedha.
- Kuchunguza sekta zenye fursa kubwa kama
utalii, kilimo, madini, dawa, fintech, na viwanda.
- Kujifunza mbinu mpya za biashara na
uwekezaji kupitia mijadala ya kitaalamu na maonesho ya bidhaa.
- Kupanua masoko ya kimataifa kwa
bidhaa na huduma za Tanzania na Misri.
Kwa kushiriki, wadau
wanajiweka katika nafasi ya kufaidika na mikakati mipya ya maendeleo,
kuimarisha ushindani wa biashara, na kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa
kikanda na kimataifa.
Jiunge nasi Cairo,
Misri tarehe 8–9 Juni 2026 na uwe sehemu ya historia ya ushirikiano wa
kiuchumi kati ya Tanzania na Misri.