TANTRADE, CLOUDS MEDIA GROUP KUINUA BIDHAA ZA MADE IN TANZANIA KIMATAIFA
- November 17, 2026
Dar es salaam.
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imekutana na uongozi wa Clouds Media Group Mkurugenzi kujadili namna ya kushirikiana katika kutangaza na kukuza utambulisho wa bidhaa za Kitanzania kupitia Nembo ya Made in Tanzania. Kikao hicho kiliongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Ephraim Balozi Mafuru pamoja na uongozi wa Clouds Media Group ukiongozwa na Mkurugenzi wa Biashara na Maendeleo, Sheba Kusaga, kikilenga kuweka msingi wa ushirikiano utakaotumia nguvu ya vyombo vya habari kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuongeza uelewa kuhusu bidhaa zinazozalishwa nchini.
Kupitia ushirikiano huo, Clouds Media Group itakuwa sehemu ya juhudi za kuhamasisha matumizi ya bidhaa za Kitanzania na kuongeza mwonekano wa wazalishaji wa ndani kupitia majukwaa yake mbalimbali ya habari na burudani. Ushirikiano huu unatarajiwa kuchochea mwamko wa wananchi kuthamini bidhaa za ndani na kuimarisha ushindani wake katika soko, sambamba na kukuza utambulisho wa bidhaa za Tanzania kupitia Nembo ya Made in Tanzania.