TANTRADE, BEVAC, ITC NA ENABEL ZAJIPANGA KUCHECHEMUA UFUGAJI WA NYUKI TANZANIA
- March 15, 2025

14, Machi 2025.
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imekutana na ITC, BEVAC NA ENABEL ambao ni wadau muhimu katika Ufugaji wa Nyuki na kuangazia maswala yenye tija katika utekelezaji wa miradi, uendelezaji wa mnyororo wa thamani katika Ufugaji wa nyuki nchini, Taasisi hizo zimejipanga vyema katika kuhakikisha uzalishaji wa asali unaongezeka kwa kiwango cha juu kupitia njia endelevu zilizoanzishwa .
Aidha Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imejipanga vyema kwa kuhakikisha mikakati thabiti inatekelezwa kwenye upatikanaji wa masoko ya mazao ya nyuki ndani na nje jambo litakalopelekea ukuwaji wa uchumi kwa wafugaji wa nyuki na kuongezeka kwa mapato ya nchi. Hayo yamebainishwa katika kikao kilichofanyika leo katika Ofisi za TANTRADE zilizopo Kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.