TANTRADE YAWANOA VIJANA 100 NAMNA YA KUYAFIKIA MASOKO YA KIMATAIFA
- November 11, 2026
10 Novemba, 2026
Arusha
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania ( TanTrade), imeshiriki katika Mdahalo wa Vijana walio katika sekta ya Kilimo kanda ya Kaskazini ikijumuisha Mikoa ya Arusha na Manyara.
Akizungumza katika Mdahalo huo, Msimamizi wa Ofisi ya Kanda, Bw. Thomas Mallya, amesema TanTrade inasaidia vijana kayafikia masoko ya kimataifa kupitia Programu mbalimbali ikiwemo Mafunzo kuhusu taratibu na vibali vinavyohitajika katika masoko ya kimataifa (Export readiness), Kutoa taarifa za biashara na kuwaunganisha na wanunuzi wa ndani na nje ya Nchi.
Kadhalika, alitoa elimu kuhusu Nembo ya Taifa ya Made in Tanzania inavyosaidia kutambulisha bidhaa kwenye masoko na kupata wateja wapya. Jumla ya Vijana 100 wameweza kunufaika na elimu hiyo.