Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YASHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 72 YA MAPINDUZI MATUKUFU YA ALGERIA

  • November 25, 2026

25 Novemba 2026
Dar es Salaam

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeshiriki hafla ya kumbukizi ya miaka 72 ya mapinduzi matukufu ya Algeria iliyofanyika katika ofisi za ubalozi wa Algeria nchini Tanzania, jijini Dar es Salaama. 

Akiongea katika hafla hiyo mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba (Mb), amesema Tanzania itaendelea kushirikiana kwa karibu na nchi ya Algeria katika masuala muhimu ya kidiplomasia na uchumi, ikiwemo ukuzaji wa biashara na upatikanaji wa masoko ya uhakika kwa wazalishaji wa Tanzania. Aidha, amesema mahusiano kati ya Tanzania na Algeria umejengwa na misingi imara iliyowekwa katika utamaduni, siasa na uchumi. 

Mwakilishi wa TanTrade, Meneja wa Masoko ya Ndani na Nje ya Nchi, Bi. Doroth Urio ameeleza kuwa  TanTrade itaendelea kujenga ushirikiano imara katika biashara kwa kuhakikisha kuwa bidhaa zinazozalishwa katika nchi hizo zinapata masoko yenye manufaa kwa pande zote mbili. 

Ushiriki wa TanTrade katika maadhimisho hayo ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia, kiuchumi na kibiashara ili wazalishaji na wafanyabishara wa Tanzania na Algeria pamoja waweze kutambua fursa za masoko ya bidhaa zao.