Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YARATIBU USHIRIKI WA WAJASIRIAMALI WANAWAKE 12 KATIKA TUZO ZA MALKIA WA NGUVU

  • November 14, 2026

14 Novemba, 2026
Dar es Salaam

Katika kuendeleza ushiriki wa wanawake katika biashara na kukuza uchumi, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeratibu ushiriki wa wajasiriamali wanawake 12 katika hafla ya kilele cha Malkia wa Nguvu 2026, iliyofanyika tarehe 14 Novemba 2026 katika Ukumbi wa Ocean View Arena, Kawe, jijini Dar es Salaam. Hatua hiyo inalenga kuwawezesha kupata fursa ya kujifunza kutoka kwa wanawake waliofanikiwa katika nyanja mbalimbali, kubadilishana uzoefu, kujenga mitandao ya kibiashara na kupata hamasa ya kukuza biashara zao.

TanTrade inatambua mchango muhimu wa wanawake katika ukuaji wa biashara na uchumi wa Taifa. Kupitia uratibu wa fursa kama hii, Mamlaka inaendelea kuwawezesha wanawake kushiriki majukwaa yenye tija, kuimarisha mahusiano ya kibiashara na kuunganisha juhudi zao na fursa za masoko ya ndani, kikanda na kimataifa.