Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YAHAMASISHA USAFI WA MAZINGIRA YA BIASHARA KUKUZA UCHUMI WA DAR ES SALAAM

  • November 14, 2026

Dar es salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amezindua rasmi Kampeni ya Usafi wa Jiji la Dar es Salaam katika Viwanja vya Maonesho vya Kijitonyama Posta, yenye lengo la kuhamasisha wananchi na wafanyabiashara kushiriki katika kuweka mazingira safi na salama. Kampeni hiyo inalenga kujenga jiji lenye mvuto na mazingira rafiki kwa shughuli za biashara na uwekezaji.

Katika kampeni hiyo, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeshiriki kwa kutoa elimu kwa wafanyabiashara na Wananchi kuhusu umuhimu wa kufanya biashara katika mazingira safi na yanayovutia. Kupitia elimu hiyo, wafanyabiashara wamehamasishwa kutunza maeneo yao ya biashara, kuhakikisha bidhaa zinahifadhiwa katika mazingira bora na kuzingatia usafi kama sehemu ya kuongeza thamani ya bidhaa za Tanzania.

TanTrade imesisitiza kuwa usafi wa mazingira ya biashara una mchango mkubwa katika kuvutia wateja, kujenga imani kwa bidhaa zinazouzwa na kuongeza ushindani katika soko. Hivyo, usafi haupaswi kuonekana kama jukumu la mamlaka husika pekee, bali ni wajibu wa kila mfanyabiashara na mwananchi katika kujenga jiji safi litakalochochea ukuaji wa biashara na uchumi.