TANTRADE YAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI YA USHIRIKI WA SEKTA ZA UMMA ZITF 2027
- November 19, 2026
Dar Es Salaam
19 Novemba, 2026
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Biashara wa mamlaka ya maendeleo ya biashara (TanTrade), Lulu Mkude, leo Novemba 19, 2026, ameongoza kikao cha wataalamu cha maandalizi ya ushiriki wa sekta za umma katika Maonesho ya 13 ya Kimataifa ya Biashara (ZITF 2027).
Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Samia uliopo ndani ya Viwanja vya Sabasaba, Makao Makuu ya Mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania (TanTrade), jijini Dar es Salaam, na kushirikisha baadhi ya wajumbe kutoka TanTrade Bara na visiwani Zanzibar pamoja na taasisi mbalimbali kutoka wizara za viwanda na biashara, kilimo, mali asili na mifugo na wizara nyingine mbalimbali.
Kikao hicho ni sehemu ya maandalizi ya awali yenye lengo la kuratibu na kuweka mikakati ya ushiriki wa sekta za umma katika maonesho hayo ya kimataifa, ili kuhakikisha taasisi zinazohusika zinajiandaa ipasavyo na kutumia fursa hiyo kutangaza huduma, bidhaa, uwekezaji na uwezo wa Tanzania katika masoko ya kimataifa.
Kupitia kikao hicho, wataalamu wamejadili masuala mbalimbali ya maandalizi, uratibu na namna ya kuhakikisha ushiriki wa sekta za umma unakuwa wenye tija, unaoendana na malengo ya maonesho pamoja na kukuza mahusiano ya kibiashara na ushirikiano wa kimataifa.
Maonesho ya ZITF ni maonesho muhimu ya biashara yanayowakutanisha wadau kutoka nchi mbalimbali, kutoa fursa za kutangaza bidhaa na huduma, kujenga mitandao ya kibiashara na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi baina ya Tanzania na mataifa mengine.