Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YAKABIDHIWA VIFAA VYA MAONESHO NA UBALOZI WA KOREA NCHINI

  • April 13, 2024

19 Machi 2024
Dar es salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi Latifa M. Khamis siku ya leo ameongoza zoezi la makabidhiano ya vizimba vya maonesho pamoja na vitendea kazi ambavyo vitatumika katika maonesho mbalimbali ya kibiashara kutoka kwa Ubalozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzania.

Katika halfa hiyo Bi. Latifa amekabidhiwa vizimba na vifaa mbalimbali vya utendaji kazi na balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzania, Balozi Kim Sun Pyo.

Aidha Bi. Latifa amesema kuwa
kupitia vifaa hivyo walivyopokea kutoka Jamhuri ya Korea kupitia TANTRADE vitaongeza pato la taifa kwani kutakuwa na ufanisi mkubwa wa utendaji kazi, aidha kupitia matumizi ya Skana mpya 30  kutaleta urahisi wa kuhudumia wadau na wananchi kwa haraka, hususan kipindi cha Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam maarufu kama (Sabasaba)