Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YASHIRIKI KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA INDIA

  • October 10, 2023

Tarehe 10 Octoba, 2023.
Delhi.
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)  imeshiriki kwenye  Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na India lililofanyika tarehe 10 Octoba, 2023 katika jiji la  Delhi.
Kongamano hilo ni sehemu ya Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ilioanza tarehe 08 - 11 Octoba, 2023 yenye lengo la kuendeleza na kukuza mahusiano ya kihistoria kati ya nchi hizi na hasa kuhamasisha biashara na Uwekezaji kwa pande zote mbili.
Taasisi mbalimbali za  Sekta Binafsi na Umma pamoja na wafanyabiashara kutoka Tanzania wamekutana na wenzao wa India kubadilishana fursa baina yao.

Katika  Kongamano hilo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wafanyabiashara wa  India na Tanzania mazingira mazuri yatakayoendelea kukuza  biashara baina ya nchi hizi mbili ikiwa ni pamoja na sera thabiti.
Aidha kwa
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi.Latifa Mohamed Khamis amesema kuwa , TanTrade itaendelea itaendelea kuibua fursa kwa wadau wa biashara nchini na kuratibu mikutano ya Biashara na kuhakikisha wafanyabiashara wa Tanzania wanaunganishwa na wafanyabiashara wa India ili kupata soko la bidhaa na kuendeleza Biashara hizo.
Katika kongamano hilo kulikuwa na mabadilishano ya makubaliano ambayo chimbuko lake ni Siku ya  Hariana Day iliyoratibiwa kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam.