Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YASHIRIKI URATIBU WA MAONESHO YA BIASHARA YA MIAKA 60 YA MUUNGANO

  • April 15, 2024

14 April,2024
Nyamazi Zanzibar

Maonesho ya Biashara ya Miaka60 ya Muungano yanayojumuisha Taasisi za Jamhuri ya Muungano Tanzania, Makampuni na Wajasiriamali yamefunguliwa siku ya leo katika viwanja vya maonesho Nyamanzi, mkabala na Fumba Town Zanzibar.  

Katika ufunguzi huo TanTrade ilikuwa sehemu ya Uratibu wa ufunguzi huo ambapo  Mgeni Rasmi katika sherehe hizo alikuwa Mheshimiwa Raisi wa Zanzibar Dr. Hussein Ali Mwinyi ambaye amefanya ufunguzi huo rasmi leo tarehe 14 Aprili, 2024.

Maonesho haya yanayohusisha Wizara, Taasisi, Kampuni na wajasiriamali kutoka Tanzania bara na Zanzibar yatadumu kwa kipindi cha siku saba na yatafungwa rasmi tarehe 20 Aprili 2024