TANTRADE YASHIRIKI KATIKA MAONESHO YA 27 YA MEDEXPO DAR ES SALAAM
- September 4, 2026
Dar es Salaam, Septemba 3, 2026
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) inashiriki katika Maonesho ya 27 ya Afya na Vifaa Tiba (MEDEXPO), yanayofanyika kuanzia Septemba 2 hadi 4, 2026 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Ushiriki wa TanTrade katika maonesho hayo unatoa fursa kwa watembeleaji kupata taarifa kuhusu majukumu yake katika kuwezesha na kukuza biashara, kutafuta na kuendeleza masoko ya bidhaa za Tanzania, pamoja na kuwafahamisha wafanyabiashara na wazalishaji kuhusu fursa mbalimbali za kibiashara zinazopatikana ndani na nje ya nchi.
Pia TanTrade Katika maonesho hayo inatoa elimu kwa watembeleaji kuhusu Nembo ya Taifa ya Made in Tanzania, umuhimu wa kuitumia katika bidhaa zao, pamoja na namna nembo hiyo inavyoweza kusaidia katika kuitambulisha na kuitangaza bidhaa ya Kitanzania katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
Aidha, ushiriki huo unalenga kuongeza uelewa kwa wadau wa sekta ya afya, wazalishaji na wafanyabiashara kuhusu fursa za masoko zinazopatikana ndani na nje ya Tanzania, huku ukiwapa nafasi ya kupata taarifa na ushauri unaoweza kuwawezesha kukuza biashara zao.