Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YASHIRIKI MAFUNZO YA USIMAMIZI WA VIHATARISHI KATIKA UDHIBITI WA MIPAKA NA UWEZESHAJI BIASHARA

  • October 22, 2026



20 Oktoba 2026, Dar es Salaam

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeshiriki mafunzo ya Usimamizi Jumuishi wa Vihatarishi kwa taasisi zinazohusika na udhibiti wa mipaka na biashara nchini. Mafunzo hayo yanalenga kuimarisha uwezo wa kutambua, kutathmini na kudhibiti vihatarishi, sambamba na kurahisisha biashara na kuongeza ufanisi wa huduma mipakani.

Mafunzo hayo yanaungwa mkono na Kituo cha Kimataifa cha Biashara (ITC) kupitia Programu ya MARKUP II, kwa uratibu wa Wizara ya Viwanda na Biashara kupitia Sekretarieti ya Kamati ya Kitaifa ya Uwezeshaji Biashara (NCTF). Washiriki wanajifunza mbinu za tathmini ya vihatarishi, matumizi ya takwimu katika kufanya maamuzi na teknolojia zinazosaidia kuboresha mifumo ya udhibiti.

Akizungumza katika mafunzo hayo, mwakilishi wa TanTrade amesisitiza umuhimu wa kutumia mifumo ya udhibiti inayozingatia kiwango cha vihatarishi ili kupunguza ukaguzi usio wa lazima, urudufu wa taratibu na ucheleweshaji wa mizigo. Ameeleza kuwa mbinu hiyo inaziwezesha taasisi kuelekeza rasilimali katika mizigo yenye vihatarishi vikubwa na kuharakisha upitishaji wa mizigo yenye vihatarishi vidogo, huku zikilinda afya ya umma, usalama wa bidhaa, ukusanyaji wa mapato na usalama wa Taifa.

Aidha, TanTrade imehimiza taasisi husika kuimarisha ushirikiano, ubadilishanaji wa taarifa na uratibu wa ukaguzi ili kuongeza ufanisi wa huduma mipakani. Kwa wafanyabiashara, maboresho hayo yanalenga kupunguza muda na gharama za kusafirisha bidhaa, kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania na kurahisisha ufikiaji wa masoko ya kikanda na kimataifa