Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YAKABIDHIWA RASMI BANDA LA TANZANIA, EXPO 2023 DOHA, QATAR

  • October 9, 2023

Mamalaka ya Maendeleo ya BiasharaTanzania (TanTrade) imekabidhiwa rasmi banda la Tanzania katika Maonesho ya Dunia ya Bidhaa za Mbogamboga na Matunda (Horticultural Expo 2023 Doha, Qatar) yanayofanyika Doha nchini Qatar. TanTrade imewakilishwa na Bw. Baltazari Erro na Bw. Baraka Peter kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade ambaye pia ni Kamishna Jenerali kwa Upande wa Tanzania katika Maonesho hayo.

Maonesho hayo yanafanyika kuanzia tarehe 02 Oktoba 2023 hadi 28 Machi 2023. Kauli mbiu ya Maonesho hayo ni Green 'Desert Better Environment"/ Jangwa la Kijani, Mazingira Bora ikilenga kuhamasisha kilimo cha Matunda na Mbogamboga kwenye mazingira ya jangwa ili kupunguza kuenea kwa jangwa

Tanzania ni miongoni mwa nchi 88 zinazoshiriki katika Maonesho hayo ikitarajia kutangaza fursa mbalimbali za Biashara, Utalii, Kilimo na Uwekezaji.

#TukutaneExpoDoha2023