TANTRADE NA TPSF KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA KUKUZA BIASHARA NA KUENDELEZA SEKTA BINAFSI
- November 17, 2026
17 Novemba, 2026
Dar es Salaam
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) zimesaini hati ya Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) yenye lengo la kuimarisha ushirikiano katika kukuza na kuendeleza biashara ya ndani na kimataifa pamoja na kuimarisha mchango wa sekta binafsi katika maendeleo ya uchumi wa Taifa.
Kupitia makubaliano hayo yaliyofanyika katika Ofisi za TPSF, Dar es Salaam, taasisi hizo zinalenga kushirikiana katika maeneo muhimu yakiwemo, kukuza biashara ya ndani na kimataifa, Kuimarisha na kuongeza mauzo ya nje ya bidhaa na huduma za Kitanzania, Kupanua fursa za masoko ya kikanda na kimataifa kwa wafanyabiashara wa Kitanzania, Kuwezesha upatikanaji wa taarifa za masoko na fursa za biashara, kuimarisha uwezo na ushindani wa wafanyabiashara, wajasiriamali na sekta binafsi kwa ujumla.
Aidha, ushirikiano huu unalenga katika Kukuza ushiriki wa sekta binafsi katika shughuli za biashara na Kuimarisha maslahi ya sekta binafsi kwa kuboresha mazingira ya biashara nchini.
Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa Makubaliano, Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Ephraim Balozi Mafuru amesema, ushirikiano wa TanTrade na TPSF ni sehemu ya juhudi za kuchangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayolenga kuijenga Tanzania yenye uchumi imara, jumuishi, shindani unaoongozwa na uuzaji wa bidhaa za nje kutoka dola bilioni 19.98 mwaka 2026 na kufikia dola bilioni 220 mwaka 2050.
Amesema sekta binafsi ina mchango muhimu katika kufanikisha Dira ya 2050 kupitia uwekezaji, uzalishaji wa bidhaa bora, upanuzi wa masoko, ajira na ubunifu. Alisisitiza kuwa ushirikiano wa TanTrade na TPSF utaimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji, kuongeza mchango wa sekta binafsi katika uchumi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Bw. Deogratius Massawe amesema, Ushirikiano huu ni hatua muhimu katika kuunganisha nguvu na rasilimali za taasisi hizo kwa lengo la kujenga sekta binafsi imara na yenye ushindani ili kuchochea ukuaji endelevu wa uchumi wa Taifa.