TANTRADE KUENDELEA KUWAWEZESHA VIJANA KUFIKIA FURSA ZA MASOKO YA NDANI NA KIMATAIFA
- November 21, 2026
20 Novemba, 2026
Dar Es Salaam
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TAnTrade) imeshiriki katika Kongamano la Uwekezaji la Vijana (Youth Investment Forum) liliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya CRDB, jijini Dar es Salaam, tarehe 20 Novemba 2026.
Kongamano hilo limefunguliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka, ambaye aliwahimiza vijana kutumia fursa za uwekezaji, mitaji, teknolojia na masoko zinazopatikana ili kuanzisha biashara, kuzalisha bidhaa na huduma, kuajiri wengine na kuchangia mapato ya Taifa, ili kutimiza Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Ushiriki wa TanTrade unalenga kutoa elimu kwa vijana kuhusu huduma wezeshi za biashara zinazoratibiwa na Mamlaka ikiwemo fursa za biashara na masoko.
Akizungumza katika Kongamano hilo, mwakilishi wa TanTrade, Afisa Mwandamizi kutoka kitengo cha Taarifa za Biashara na Masoko, Bi. Lulu Masanja, ameeleza kuwa TanTrade itaendelea kuhakikisha inawasaidia vijana wajasiriamali kupata masoko ya ndani na kimataifa kupitia hatua za kutoa bidhaa ya Kitanzania kutoka soko la ndani kwenda masoko ya kikanda na kimataifa, pamoja na elimu mbalimbali zinazolenga biashara ndogo na za kati zinazomilikiwa na vijana.
Kadhalika, amewasisitiza vijana kuendelea kutumia fursa za maonesho, mikutano na makongamano ya kibiashara ili kuwafikia wanunuzi, kuongeza ujuzi na ubunifu pamoja na kutumia teknolojia wezeshi za kukuza biashara zao.
Kwa upande wa viongozi wa vijana kutoka Youth Investors Association (YIA) wamsisitiza vijana kuongeza ushiriki katika kujadili shughuli za kiuchumi na biashara.
TanTradre itaendelea kuwawezesha na kuwajengea uwezo vijana waweze kutumia fursa mbalimbali za biashara ili kukuza, kuendeleza biashara na kupanua masoko ya bidhaa zao.