TANTRADE KUENDELEA KUWAUNGANISHA WAZALISHAJI WA BIDHAA NA WANUNUZI
- November 14, 2026
13 Novemba 2026
Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Ephraim Balozi Mafuru, amesema kuwa TanTrade itaendelea kuwaungamisha wazalishaji bidhaa na wanunuzi ikiwa ni sehemu ya msingi katika utekelezani wa majukumu yake, ili kuwa na masoko ya uhakika.
Amesema hayo katika Kongamano la Saba la Masoko na Tuzo (TMA) 2026, lililoandaliwa na Chama cha Wataalamu wa Sayansi ya Masoko Tanzania (TMSA), jijini Dar es Salaam.
Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za TanTrade katika kukuza biashara na kuhakikisha wazalishaji wanapata masoko ya uhakika ndani ya nchi, kikanda na kimataifa, hivyo kuongeza ushindani na upatikanaji wa masoko mapya kwa bidhaa za Tanzania.