Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YAALIKWA NA SERIKALI YA JIMBO LA HARIANA

  • October 13, 2023

Katika muendelezo wa mahusiano kati ya TanTrade na Jimbo la Hariana nchini India, leo tarehe 13 Oktoba 2023, Ujumbe wa TanTade ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Latifa Mohamed Khamis ulialikwa na Serikali ya jimbo la Haryana India kutembelea viwanda mbalimbali lakini pia kufanya mazungumzo na wawekezaji kutoka jimbo hilo.

TanTrade ilipata fursa pia ya kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wakubwa kutoka Japan walioongozwa na Waziri wa Japan wa Biashara ambaye alihudhuria kwa njia ya mtandao.

Serikali ya Haryana pamoja na wafanyabiashara na wawekezaji wa India wenye asili ya Japan kupitia Chemba ya Japan ya Biashara na Viwanda ya India zimeonesha nia ya dhati ya kuja kuwekeza Tanzania na hivi karibuni wataanza kutuma wawakilishi mbalimbali kwa hatua mbalimbali.

Mualiko huo ni matokeo mazuri yaliyotokana na kazi kubwa na Ziara ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoifanya katika kuimarisha mahusiano na serikali ya India.