WATUMISHI WA TANTRADE WAPONGEZWA NA KUHIMIZWA KUENDELEA KUFANYA KAZI KWA BIDII
- November 10, 2025
6 Novemba, 2025
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Dkt. Latifa M. Khamis amewapongeza Watumishi na timu za Ulinzi na Usalama ,Watumishi wote kwa kutimiza haki yao ya msingi ya kuchangua Viongozi wa nchi.
Aidha Dkt. Latifa alisisitiza upendo, msamaha, bidii na kuwa wabunifu ili kuendelea kuijenga TanTrade kwa maslai mapana ya Taifa. Ameyasema hayo alipokua akiongea na Watumishi katika Ukumbi wa Kilimanjaro uliopo katika Uwanja wa Mwl J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam.