Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YARATIBU KONGAMANO LA KIBIASHARA NCHINI MALAWI

  • July 21, 2023


____________________

Na. Norah Thomas-Mzuzu, MALAWI
26 Aprili 2023


Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania Kwa kushirikiana na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania- Malawi na Kituo cha Uwekezaji (TIC) imeratibu Msafara wa Kibiashara uliohusisha Wafanyabiashara Wakati na Wadogo 150 kutoka Tanzania,

Mkuu wa Msafara huo ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara aliyemwakilisha Mhe.Waziri Dkt. Ashatu Kijaji ambaye aliambatana na Taasisi mbalimbali za serikali na binafsi pamoja na Makampuni.

Akizungumza katika kongamano hilo, Waziri wa Viwanda na Biashara wa Malawi Mhe. Simplex chithyola Banda, ameelekeza Kituo Cha Biashara Malawi kushirikiana na Tanzania kuandaa kongamano Kila baada ya Muda mfupi tofauti na kipindi Cha Miaka mitano tangu lifanyike la kwanza upande wa Tanzania.

Mhe. Waziri Amewataka Wafanyabiashara kutumia fursa na mahusuano mazuri kuboresha Biashara.

Naye katulibu Mkuu Dkt. Hashil Abdalah amewajakikishia wafanyabiashara kupata ushirikiano wa kutosha Kwa kuwa mazingira ya Biashara yameboreshwa na Taasisi zake zote ikiwemo TanTrade zipo tayari kutua muongozo na Taarifa za Biashara.

Kongamano hili linalotarajiwa kuhitimishwa tarehe 28 Aprili, 2023 limeambatana na Maonesho ya bidhaa za Tanzania na Malawi.