TANTRADE NA WRRB KUTOA MAFUNZO YA MFUMO WA STAKABADHI ZA GHALA
- August 29, 2023

..........................
Na. Norah Thomas-TanTrade
Dar es salaam.
28 Agosti 2023.
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa kushirikiana na BODI ya usimamizi wa stakabadhi za ghala (WRRB) Tarehe 28 Agosti 2023 watoa Mafunzo ya utekelezaji wa mfumo wa stakabadhi za ghala yenye lengo la kuwajenga uwezo Watendaji wa Kampuni za waendesha ghala, Wasimamizi wa Ghala, Meneja Dhamana pamoja na washiriki binafsi, Mafunzo yatadumu kwa muda wa siku 5 kuanzia Tarehe 28 Agosti mpaka Tarehe 1 septemba 2023.
Akizungumza katika Mafunzo hayo, Mkuu wa wilaya ya Ubungo, Hashim Komba katika ukumbi wa Kilimanjaro uliopo katika Uwanja wa Maonesho ya Sabasaba,alisema mafunzo hayo yanakwenda kuongeza heshima kwa watendaji wa ghala na kupelekea utoaji wa huduma bora kwa Wadau wote.
Amesema bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala inatakiwa kuongeza matumizi ya TEHAMA katika utendaji ili kuendana na mabadiliko ya dunia.
Naye Mkurugenzi wa huduma za uendeshaji wa Biashara kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi. Mary Fidelis amesema kuwa TanTrade ipo tayari kutoa ushirikiano wa kiutendaji ili kuwajengea uwezo Watendaji wa Kampuni za waendesha ghala, Wasimamizi wa Ghala, Meneja Dhamana pamoja na washiriki binafsi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Stakabadhi za Ghala Asangye Bangu amesema kuwa lengo kubwa la mafunzo hayo ni kuongeza tija katika ufanyaji kazi na matarajio ya mafunzo hayo ni kuhakikisha kazi zinafanywa kwa usahihi kwa kuzingatia sheria .
Bangu ameongeza kuwa Bodi ya Udhibiti na Usimamizi wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala imejipanga kuona ambavyo watendaji hao watatekeleza shughuli zao za kiserikali kwani wamejitaidi kuingiza bidhaa mbalimbali kadiri sheria ilivyo waruhusu kufanya hivyo.
‘’nilipofanya ukaguzi nilibaini changamoto mbalimbali kwenye maghala, anaeshikiliwa kwanza ni Meneja na Mkurugenzi anakuwa hayupo ukimuuliza Mkurugenzi anakuambia Meneja wangu ndio anaehusika, kwahiyo mda mwingine unakuta meneja hana Taharifa, hivyo natoa wito kwa Washiriki wote kuzingatia Mafunzo yanayotolewa ili kuwaongezea uwezo wa Kiutendaji. Alisema