Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE NA TANROADS WABORESHA MIUNDO MBINU YA BARABARA KATIKA UWANJA WA MAONESHO YA SABASABA.

  • July 24, 2023




---------------------

15 Juni, 2023
Dar es Salaam

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)  na  Wakala wa Barabara Tanzania (TanRoads)  kuboresha na kukarabati miundo mbinu ya ndani na nje ya Uwanja wa Maonesho wa mwl. J.K Nyerere uliopo barabara ya Kilwa Dar es salaam.


Kikao kazi  hicho 
kimefanyika 15 Juni, 2023,  katika ofisi za TanTrade Dar es salaam na kuhudhuliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania bi. Latifa M. Khamis, na Wataalam  kutoka Tanroads Mhandisi Haruin Rashid Senkuku, Mhandisi Elisony Edward Mweladzi, Mhandisi Raymond Godfrey Maimu pamoja na wajumbe wa mkutano huo kutoka TanTrade.

Akiongea katika kikao hicho, bi. Latifa amesema tumeamua kushirikiana na Tanroads katika kuboresha miundo mbinu ya Uwanja ili kuchochea mabadiliko makubwa na kuyapa zaidi mvuto maonesho ya mwaka huu pamoja na kuleta urahisi wa kufanya biashara.

 "Lengo ni kuendelea kuboresha miundombinu ya Maonesho ili kuweka mazingira mazuri kaa ya uoneshaji wa bidhaa kwa Wafanyabiashara pamoja na Watembeleaji na kuleta matokeo yenye tija" alisema.