Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE NA EXPO LINK WAKUBALIANA KUKUZA NA KUENDELEZA BIASHARA TANZANIA.

  • July 25, 2023



Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TanTrade) kwa kushirikiana na kampuni ya  Expo Link kutoka Misri Leo tarehe 18 Julai 2023 imefanya mkutano wa Kibiashara Zanzibar.
Mkutano huo uliwakutanisha wafanyabiashara kutoka Misri na Tanzania kwenye sekta ya Samani za Majumbani, Vifaa vya mahoteli , vifaa vya majumbani, TEHAMA na biashara za Huduma za kihoteli.

Wafanyabiashara wapatao 125  ambapo kutoka Tanzania 95 na Misri 25 walishiriki B2B hiyo ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Balozi wa Misri ,Mheshimiwa Balozi Sherif Ismail akiambatana na Balozi wa Tanzania Nchini Sudan Balozi Silima pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE  Bw Freddy Liundi.