Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE NA UBALOZI WA IRAN YAENDELEA KUIMARISHA MAHUSIANO YA BIASHARA NA UWEKEZAJI.

  • July 24, 2023



23 Juni, 2023
Dar es salaam

Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi.Latifa M. Khamis amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Balozi Hussein Alvandi Behineh, Balozi wa Iran nchini yaliyofanyika katika Ofisi za Balozi tarehe 23 Juni, 2023.

Lengo la kikao hicho ni kujadili ukuzaji wa mahusiano ya kibiashara baina ya Tanzania na Iran Katika Biashara na Uwekezaji kwa Sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na afya, elimu na teknolojia.

Katika kikao hicho wamejadili kuhusu ushiriki wa Iran kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ambapo kutakuwa na siku maalum ya Iran kwa ajili ya kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na Iran ili kubadilishana fursa baina yao.
Sambamba na hilo walijadili kuhusu kuratibu misafara ya kisekta zikiwemo afya, elimu na teknolojia mbalimbali.