Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YASHIRIKI KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA INDONESIA

  • January 25, 2024

Jakarta, Indonesia
25 Januari, 2024.

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)  imeratibu na kushiriki kwenye  Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Indonesia lililofanyika tarehe 25 January, 2024 katika jiji la  Jakarta.

Kongamano hilo ni sehemu ya Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ilioanza tarehe 24 January, 2024 yenye lengo la kuendeleza na kukuza mahusiano ya kiuchumi kati ya nchi hizi na hasa kuhamasisha biashara na Uwekezaji kwa pande zote mbili.

Taasisi mbalimbali za  Sekta Binafsi na Umma pamoja na wafanyabiashara kutoka Tanzania wamekutana na wenzao wa Indonesia kubadilishana fursa baina yao.

Katika  Kongamano hilo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wafanyabiashara wa  Indonesia na Tanzania mazingira mazuri yatakayoendelea kukuza  biashara baina ya nchi hizi mbili ikiwa ni pamoja na sera thabiti za kisiasa na uchumi.

Aidha kwa
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Bi.Latifa Mohamed Khamis pamoja na Bw. Soegeng Hernowo, Mkurugenzi Mkuu wa PT PPI walisaini na kubadilishana hati ya makubaliano ya ushirikiano katika ukuzaji biashara kwa nchi zote mbili.

Mkurugenzi wa TanTrade pia alitumia fursa hiyo kuainisha fursa za biashara zilizopo Tanzania na kueleza kuwa TanTrade itaendelea  kuibua fursa kwa wadau wa biashara nchini na kuratibu mikutano ya Biashara na kuhakikisha wafanyabiashara wa Tanzania wanaunganishwa na wafanyabiashara wa Indonesia ili kupata soko la bidhaa zinazozalishwa nchin