Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

Kikao cha Kimkakati Kati ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania na Idara ya Uhamiaji

  • April 17, 2026

Kikao cha Kimkakati kati ya TanTrade na Idara ya Uhamiaji

Tarehe 16 April 2026, Dar es Salaam

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imefanya kikao cha kimkakati na Idara ya Uhamiaji kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma na kuimarisha mazingira ya biashara nchini. 

Mazungumzo haya yamejikita katika maeneo muhimu yafuatayo:
a)       Uratibu wa misafara ya kibiashara ndani na nje ya nchi ili kurahisisha safari za wafanyabiashara na wawekezaji, huku taratibu za uhamiaji zikiboreshwa kwa ufanisi na usalama.
b)       Kuimarisha makongamano na mikutano ya kimataifa kwa kuhakikisha usalama wa wageni wa kimataifa na Watanzania wanaoshiriki katika majukwaa ya nje ya nchi, ili kulinda maslahi ya taifa na kuimarisha diplomasia ya kiuchumi.
c)       Kuboresha maandalizi ya maonesho ya biashara ya kimataifa na dunia (EXPOs) yanayofanyika Tanzania na nje ya mipaka, kwa kuweka mifumo thabiti ya usalama na huduma bora kwa washiriki.
d)       Kujenga mazingira rafiki ya biashara kwa kushirikisha taasisi muhimu katika kukuza shughuli za kibiashara na uwekezaji, na kuhakikisha Tanzania inakuwa kitovu cha mikutano na maonesho yenye tija na manufaa kwa uchumi wa taifa.

Kikao hiki kimeweka msingi wa ushirikiano wa karibu kati ya TanTrade na Idara ya Uhamiaji, ambacho kitasaidia:
a)       Kuimarisha usalama wa Watanzania wanaoshiriki mikutano na makongamano nje ya nchi, kwa kuhakikisha wanapata ulinzi wa kisheria na kiutawala wanapokuwa katika majukwaa ya kimataifa.
b)       Kuongeza mapato ya taifa kupitia sekta ya biashara, utalii wa mikutano (MICE), na uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni.
c)       Kuweka Tanzania katika nafasi ya kipekee kama kituo ya kimataifa ya biashara na uwekezaji, yenye usalama, tija na manufaa kwa uchumi wa taifa.

Kikao cha kimkakati kati ya TanTrade na Idara ya Uhamiaji kimeweka msingi wa ushirikiano thabiti unaolenga kurahisisha safari za kibiashara, kuimarisha maandalizi ya maonesho na mikutano ya kimataifa, na kujenga mazingira rafiki ya uwekezaji, huku kikipa kipaumbele kwa usalama wa wageni wanaokuja Tanzania na Watanzania wanaoshiriki mikutano nje ya nchi, hatua inayojenga taswira ya taifa kama kitovu cha biashara na uwekezaji barani Afrika.