Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

Uchambuzi wa Takwimu uliofanywa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)

  • September 6, 2023

DAR ES SALAAM: Uchambuzi wa Takwimu uliofanywa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), umebainisha bidhaa tisa za Tanzania zinazohitajika zaidi katika masoko mbalimbali duniani.

Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade, Latifa Mohammed Khamis ameeleza hayo mkoani Dar es Salaam katika taarifa yake aliyoitoa kuhusu utekelezaji wa majukumu ya mamlaka.

Amesema katika uchambuzi huo, Tantrade imezitambua bidhaa za dhahabu, korosho, ufuta, mbaazi, kahawa, dengu, pamba, almasi na vifungshio vya mifuko ndio mahitaji makuu duniani.

Amezitaja nchi ambazo zinahitaji bidhaa hizo kuwa ni India, Umoja wa Falme za Kiarabu, Uswisi, Vietnam, China, Pakistani, Japani, Marekani, Oman, Qatar, Kuwait na Saudi Arabia.

Amesema dhahabu mauzo halisi ni dola za kimarekani milioni 2,100 lakini mahitaji katika nchi hizo ni dola za kimarekani 3,400.

Vile vile mauzo halisi ya korosho ni dola za kimarekani 304 lakini fursa iliyopo ni 819.

“Mauzo halisi ya ufuta ni dola za kimarekani milioni 152 lakini fursa iliyopo ni dola za kimarekani milioni 207,” amesema.

Pia kuhusu mbaazi mauzo halisi ni dola za kimarekani 95 ila fursa iliyopo ni dola za kimarekani milioni 201.

Bidhaa nyingine ni kahawa ambayo mauzo halisi ni dola za kimarekani 157 lakini fursa iliyopo ni dola za kimarekani 171.

Kuhusu dengu mauzo halisi ni dola za kimarekani 64 ilhali fursa iliyopo ni dola za kimarekani 154.

Amesema kuwa mamlaka hiyo inaendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi ili kufikia azma ya serikali kuwa kitovu cha biashara kwa kuendeleza, kukuza na kutangaza bidhaa na huduma ndani na nje ya nchi.

Imeandaliwa na Lucy Ngowi