RAIS MWINYI: CHINA NI MSHIRIKA MUHIMU KWA UCHUMI WA ZANZIBAR
- November 8, 2024

8, November 2024.
SHANGHAI, CHINA
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema kwa kipindi cha miaka mingi, China imekuwa mshirika muhimu katika ukuaji wa uchumi Zanzibar kupitia uwekezaji na sekta mbalimbali hususan miradi ya ujenzi wa miundombinu. China ina jumla ya miradi 17 ya uwekezaji iliyosajiliwa Zanzibar yenye thamani ya takriban dola za Kimarekani milioni 245, ambayo imetoa ajira za moja kwa moja kwa wananchi wa Zanzibar zipatazo 8,000.
Aidha, China ni mshirika wa pili kwa ukubwa katika uagizaji wa bidhaa kutoka Zanzibar, ambapo thamani ya biashara baina ya nchi hizo mbili imepanda kwa kasi kufikia dola milioni 66.5 mwaka 2023. Ushirikiano huu umetoa mchango mkubwa kwa kukuza sekta za kilimo, viwanda, na biashara.
Rais. Dk. Mwinyi ameyasema hayo katika Warsha maalum ya kukuza Uwekezaji, Biashara na Utalii.