KIKAO CHA MAANDALIZI YA KONGAMANO LA WAFANYABIASHARA WA TANZANIA NA UBELGIJI CHA FANYIKA TANTRADE
- August 23, 2024

Dar es Salaam.
21 Agosti, 2024.
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imefanya Kikao na Bw. Ivan Korsak, Kamishna wa Biashara wa Hub Brussels kuhusu maandalizi ya ziara ya wafanyabiashara na wawekazaji kutoka Ubelgiji itakayofanyika tarehe 24 – 29 Novemba, 2024 katika Ofisi za TanTrade, Dar es Salaam.
Kikao hicho kilichoongozwa na Bi. Mary Fidelis, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi .Latifa Mohammed Khamis kilijadili kuhusu ujio wa kampuni takribani 25 za Sekta mbalimbali zikiwemo uchukuzi, afya, elimu na nyinginezo kutoka Ubelgiji kwa ajili ya kukutana ana kwa ana na wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania kuendeleza ushirikiano wa kibiashara na kubadilishana fursa mbalimbali kwa pande zote mbili.
Bw. Korsak alieleza kuwa amehamasika kufika TanTrade kutokana na mafanikio mbalimbali yaliyopatikana kwa ushirikiano ambao TanTrade inatoa katika kuratibu mikutano mbalimbali ya biashara, hivyo ameomba TanTrade kuendelea kutoa ushirikiano katika Ziara ya Novemba ili iwe na manufaa kwa wafanyabiashara wote.
Bi. Mary Fidelis, akiongea baada ya kupata maelezo kutoka kwa Kamishna wa Biashara Bw Korsak alieleza kuwa TanTrade itaendelea kutoa ushirikiano katika kufanikisha Kongamano hilo kwa kuwa ni moja ya majukumu yake ya msingi.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia Wakurugenzi na Maafisa wa TanTrade, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.