Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

MAANDALIZI YA SIKU YA TANZANIA, NCHINI QATAR YASHIKA KASI

  • February 24, 2024

Doha, Qatar
23 Februari 2024

Kamishna Jenerali wa Banda la Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi wa TanTrade Bi Latifa Mohamed Khamis akiongozana na Naibu Kamishna Jenerali wa Banda la Tanzania ambaye pia ni Balozi wa Tanzania nchini Qatar Mhe. Habibu Mohamed Awesi wamefika na kukagua shughuli za maandalizi ya siku ya Tanzania katika Maonesho ya Expo2023 Doha itakayofanyika tarehe 28 Februari 2024 mjini Doha.

Katika ziara hiyo, wakuu hao wa banda la Tanzania katika Maonesho haya walionesha kuridhishwa na hatua za maandalizi zilizofikiwa hadi sasa.

Tanzania inashiriki Maonesho ya Doha Expo2023 yaliyoanza Tar 2 Octoba 2023, huku yakitegemewa kuisha tar 28 Machi 2024, Doha Qatar.