Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

KAMATI YA KITAIFA YARIDHISHWA NA MAANDALIZI YA JUBILEI YA SABASABA

  • May 14, 2026


Dar es Salaam, 13 Mei 2026

Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba Jubilee ya Dhahabu) imekutana kujadili maendeleo ya maandalizi ya maonesho haya makubwa yatakayofanyika kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai 2026 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K. Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, wajumbe walipitia mikakati ya kuboresha ubora na athari za maonesho, ikiwemo maboresho ya miundombinu, kuongeza ushiriki wa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi, pamoja na maandalizi ya programu maalum kama B2B, siku za kitaifa, tuzo, mikutano, semina, makongamano, burudani, utamaduni na sanaa. Hatua hizi zinalenga kuonesha upekee wa Jubilee ya Dhahabu na kuimarisha nafasi ya Tanzania kama kitovu cha biashara na uwekezaji.

Kamati iliridhishwa na hatua zilizofikiwa na ikasisitiza umuhimu wa ushirikiano wa wadau wote ili kuhakikisha maonesho haya ya kihistoria yanakuwa jukwaa muhimu la kuendeleza biashara, kukuza uwekezaji, kuongeza ajira, kuhamasisha ubunifu na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa. Aidha, kamati ilibainisha kuwa Sabasaba ya 50 itakuwa fursa ya kuonesha urithi wa utamaduni wa Tanzania sambamba na fursa za kisasa za biashara, hivyo kuimarisha mchango wake katika mtandao wa biashara za kikanda na kimataifa.