WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA KUANDAA SERA YA KUWAWEZESHA WABUNIFU WADOGO (STARTUPS)
- October 22, 2026
Dar es Salaam, 19 Oktoba, 2026
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius John Ndejembi, ameitaka Wizara ya Viwanda na Biashara kuandaa sera maalumu itakayowawezesha wabunifu wadogo (startups) kupata fursa za kukuza bunifu zao, kuendeleza biashara na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa.
Maelekezo hayo yametolewa leo, Oktoba 19, 2026, wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Startup uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Hatua hiyo inaonesha dhamira ya Serikali ya kutambua na kuimarisha mchango wa wabunifu wadogo katika kuibua mawazo mapya, kutatua changamoto za jamii, kutengeneza ajira na kuongeza fursa za kiuchumi nchini.
Kupitia sera hiyo, Wizara ya Viwanda na Biashara inatarajiwa kuweka mazingira wezeshi yatakayosaidia wabunifu wadogo kuendeleza mawazo yao kuwa bidhaa na huduma zenye ushindani katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
Aidha, uwezeshaji wa wabunifu hao ni muhimu katika kukuza ujasiriamali, kuongeza thamani ya bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini, pamoja na kuimarisha mchango wa sekta binafsi katika kufikia malengo ya dira ya maendeleo ya taifa ifikapo mwaka 2050.