Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

MHE. LONDO MGENI RASMI KONGAMANO LA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA UAE

  • November 25, 2026


25 Novemba 2026
Dubai, UAE

Naibu Waziri Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo, anatarajia kuwa mgeni rasmi wa kongamano la biashara kati ya Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), linalotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2026 katika Hoteli ya Movenpick , jijini Dubai.

Mhe. Londo amewasili leo katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Dubai, akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Ephraim Balozi Mafuru na kupokelewa na Bw. Omar Hassan Omar, Konseli Mkuu, Konseli Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
huko Dubai na Falme za Kaskazini (Northern Emirates).

Aidha baada ya mapokezi, Mhe. Londo aliweza kupatiwa maelezo mafupi kuhusu hatua za maandalizi ya kongamano hilo kubwa. Kongamano litafanyika 

Kongamano hilo linatarajiwa kuwakutanisha washiriki kutoka Tanzania, wadau wa biashara kutoka Dubai na maeneo mengine ya UAE, pamoja na makampuni yanayoshiriki katika Tuzo za Consumer Choice Award (CCAA) ikiwa na lengo kubwa la kufungua fursa mpya za biashara, kupanua masoko na kuvutia uwekezaji kati ya Tanzania na UAE.