TUJENGE TABIA YA KUPENDA VYA KWETU
- January 7, 2025
5, Disemba 2025.
___
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Selemani Jafo ametoa rai kwa Watanzania wote kujenga mazoea ya kupenda kutumia bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini Tanzania kwa maslahi ya ukuwaji wa sekta ya Biashara na Uchumi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. Mhe. Jafo ameyasema hayo wakati akifungua rasmi Maonesho ya 11 ya Kimataifa ya Biashara Zanzibar (ZITF) yanayofanyika katika Viwanja vya Nyamanzi, Fumba, Zanzibar.
Aidha Waziri Jafo amewaomba watembeleaji kutumia maonesho haya kupata taarifa mbalimbali za bidhaa na huduma za Kizanzibari.
Maonesho ya 11 Kimataifa ya Biashara ya Zanzibar yalianza tarehe 1 Januari na yatahitimishwa tarehe 15 Januari 2025