KLINIKI YA VIWANDA NA BIASHARA SULUHISHO LA WAFANYABIASHARA ARUSHA
- September 19, 2026
Arusha, 17 Septemba 2026
Ikiwa ni siku ya tatu tangu kuanza kwa Kliniki Maalum ya Viwanda na Biashara jijini Arusha, taasisi mbalimbali, ikiwemo Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), zinaendelea kutoa huduma za uwezeshaji na ushauri kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wanaoshiriki kliniki hiyo.
Kliniki hiyo iliyoanza tarehe 14 Septemba 2026, inatarajiwa kuhitimishwa tarehe 19 Septemba 2026, ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo wajasiriamali na wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali nchini, pamoja na kuwawezesha kupata taarifa, elimu na huduma muhimu zinazohusiana na biashara na viwanda.
Kupitia ushiriki wake, TanTrade inaendelea kutoa elimu na huduma mbalimbali zinazolenga kuwawezesha wafanyabiashara na wajasiriamali kukuza biashara zao, kutafuta masoko na kutumia fursa za biashara zinazopatikana ndani na nje ya nchi.