Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

MHE. DKT. HUSSEIN ALI MWINYI MGENI RASMI KUFUNGA MAONYESHO YA 50 YA SABASABA 2026

  • July 12, 2026

Dar es Salaam, 12 Julai 2026

Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam DITF, ni maonyesho makubwa zaidi na ya zamani zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Maonyesho haya ya kimataifa yalianzishwa mwaka 1976 na kwa miaka 50 yamekuwa jukwaa kubwa la kuonesha bidhaa za kitanzania na kimataifa, hivyo kuvutia wadau wengi kutoka soko la ndani na kimataifa.

Maonyesho hayo yamebeba kaulimbiu ya " Maonesho ya 50 ya Sabasaba - Fahari ya Tanzania

Rais wa Serikali ya Zanziba na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hassan Ali Mwinyi, ndie atakayekuwa mgeni rasm wa Maonyesho hayo yaliyoanza Tarehe 28 Juni 2026 na yatahilimishwa tarehe 13 Julai 2026, katika viwanja vya Mwl, Juliaus Nyerere, Sabasaba

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeo ya Biashara Tanzania TanTrade - Dkt Latifa Khamis, amesema kuwa, maonyesho hayo yamefanyika vizuri kwa kiwango cha kimataifa, na hivyo maandalizi ya kufunga maonesho hayo yamekamilika kwa asilimia mia moja. Aidha, alisema kuwa maonesho haya yamekuwa yakipekee na makubwa kuliko miaka ya nyuma, hivyo tutarajie sekta zote za biashara kunufaika kwa mipango mbalimbali iliyofanyika kipindi cha wiki mbili za maonesho.

Sherehe za Kufunga zitaanza saa nne asubuhi, na zitahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa.