UBALOZI WA BRAZIL WATEMBELEA TANTRADE
- July 19, 2024

Dar es Salaam.
Tarehe 19 Julai, 2024.
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) leo imepokea ugeni toka Ubalozi wa Brazil nchini Tanzania ukiongozwa na Mhe. Balozi Gustavo Nogueira
Ugeni huu uliopokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Latifa M. Khamis amelenga katika kukuza mahusiano pamoja na Biashara kati ya Tanzania na Brazil.
Akiongea baada ya mapokezi hayo Bi. Latifa amebainisha kuwa Tanzania iko tayari kushirikiana na Brazil katika kuhakikisha kwamba wafanyabiashara wa Tanzania na Brazil wanakutana na kufanya Biashara pamoja na kubadilishana uzoefu katika maeneo mbalimbali kama Sekta ya Kilimo, Miundombinu na Afya.