Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

RASIMU ZA KANUNI MPYA ZA BIASHARA 2026 ZAWASILISHWA KWA WADAU

  • March 11, 2026


 
Dar es Salaam; 11 March 2026
_____________________________________________
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) imewasilisha rasimu za kanuni mpya za biashara kwa mwaka 2026 kwa wadau, zikiwa na lengo la kuongeza ushindani wa bidhaa na Tanzania katika masoko ya ndani na ya kimataifa. Kanuni hizi zinahusu maeneo muhimu kama vile mauzo ya nje, masoko mapya, maonesho ya biashara, taarifa za masoko, kuendeleza wafanyabiashara wadogo na wa kati, pamoja na utangazaji wa bidhaa kupitia nembo ya “Made in Tanzania.”
 
Rasimu zilizopendekezwa zinajumuisha kanuni za kuratibu ushirikiano wa taasisi za Serikali na sekta binafsi, kanuni za tozo, matumizi ya alama ya rajamu ya Taifa, na kanuni za ukuzaji wa maonyesho ya biashara ili kuimarisha uwazi, utawala bora na ushindani wa bidhaa za Tanzania.
 
TANTRADE inahimiza wadau wa sekta ya biashara, uzalishaji, uwekezaji na usafirishaji kusoma rasimu hizi na kuwasilisha maoni yao kwa maslahi ya Taifa. Ushirikiano wa wadau ni msingi wa mafanikio ya mchakato huu, kwani unahakikisha kanuni zinakuwa shirikishi na zenye tija kwa manufaa ya nchi.