MAKAMPUNI KUTOKA JAMHURI YA WATU CZECH KUSHIRIKI TIMEXPO MWEZI SEPTEMBA
- August 6, 2024

5.8.2024
DAR ES SALAAM.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania Bi Latifa M. Khamis amekutana na mwakilishi wa Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa Czech nchini Tanzania Mhandisi Roman Grolig na kuangazia mkakati wa mashirika mbalimbali kutoka Czech kushiriki katika maonesho ya Viwanda (TIMEXPO) wakati alipotembelea ofisi za TANTRADE zilizopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Bi Latifa pia alitumia fursa hiyo kukaribisha makampuni mbalimbali kutoka Jamhuri ya watu wa Czech kushiriki kwenye maonesho ya 49 ya DITF 2025.
Aidha Mhandisi Groling amebainisha kuwa kampuni ya AAL itashiriki kwa kufanya maonesho ya usafiri wa anga ambapo kampuni hiyo itazindua ndege aina ya AAL 600. Maonesho ya TIMEXPO yatafanyika kuanzia tarehe 29 Septemba hadi tarehe 2 Oktoba, 2024 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl.J.K. Nyerere maarufu Sabasaba, jijini Dar es Salaam.