Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

UJUMBE KUTOKA SERIKALI YA CHINA IDARA YA BIASHARA YAJA NA FURSA TANZANIA

  • February 22, 2025

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo  ya Biashara Tanzania (TanTrade ) Bi Latifa M. Khamis amepokea ujumbe kutoka  Idara ya Biashara “Department of Commerce kutoka Serikali ya China  yenye lengo la kuimarisha ushirikiano wa kibiashara baina ya serikali zote mbili, ugeni huu umepokelewa leo tarehe 21  Februari, 2025  katika  ofisi za TanTrade zilizopo katika kiwanja cha Mwl JK Nyerere, barabara ya Kilwa Jijini Dar es salam.

Aidha  Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi Latifa  ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha kushiriki katika Kongamano la “Lake Tanganyika Business Forum”  ambalo litafanyika katika Mkoa wa Kigoma, pamoja na kushiriki Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam maarufu kama “Sabasaba“  ya mwaka 2025.