Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

Toleo la 3 la Maonesho ya Biashara ya Ndani ya Afrika

  • November 12, 2023

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeratibu ushiriki wa Taasisi za Umma, Sekta binafsi pamoja na Wafanyabiashara kwenye Maonesho ya Biashara ya kimataifa ya Afrika (3rd Edition of Intra - African Trade Fair) yaliyoanza rasmi tarehe 09 Novemba, 2023 na yatamalizika tarehe 15 Novemba, 2023 Cairo Misri.


Maonesho haya yatatoa fursa kwa wafanyabiashara wa Tanzania kuongeza wigo wa soko kwa bidhaa zao katika Soko huru la Afrika (AfCFTA) na kukuza mahusiano ya Kidiplomasia na kibiashara kwa nchi za Afrika