ZHEJIANG AFRICA (ZASC) KUANZISHA VIWANDA VYA UZALISHAJI BIDHAA NCHINI TANZANIA
- July 25, 2023

--------------------
Na. Norah Thomas-TanTrade Dar es salaam.
28 Juni 2023
DAR ES SALAAM
Kituo cha Huduma cha Zhejiang Africa (ZASC) mapema leo kimefanya uzinduzi wa banda lao katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl. JK nyerere (sabasaba) Dar es salaam, ZASC ni shirika lisilo la kiserikali lenye dhamira ya kusaidia biashara ya mashirika ya China barani Afrika kupata uelewa wa masoko pamoja na ujenzi wa mtandao wa Kibiashara katika nchi za Afrika. Aidha ZASC pia inatoa msaada kwa kampuni za Afrika ili kuzisaidia kuingia China pamoja na soko la Asia Mashariki. ZASC pia inasaidia Wanafunzi wa Afrika wa Kimataifa wanaoanzisha biashara nchini China, ikiwa ni Pamoja na kuwasaidia kujenga uhusiano na wauzaji kutoka viwandani.
Akiongea katika hafla hiyo Msemaji wa shirika Bw. Yiwei Hao, kwa niaba ya Rais bw. Qi Xie, alisema “Tumeleta zaidi ya mashirika matano (5) tofauti yakiwemo makampuni mawili ya umma (yaliyoorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Shanghai) kwenye Maonyesho ya Sabasaba, ivyo tunatoa wito kwa Wafanyabiashara, Makampuni na Taasisi mbalimbali kuudhulia Maonesho na kutembelea katika banda letu ili kujionea na kujifunza teknolojia ya kisasa ya uzalishaji bidhaa.
“Kikundi hiki cha wajumbe kina mpango wa kufanya biashara na Tanzania kama tulivyofanya biashara na nchi nyingine, na kama tunavyosambaza Dubai kuanzia sasa tutafanya biashara ya moja kwa moja kati ya China na Tanzania kuleta bidhaa zetu kwa Watanzania kwa bei nafuu kwa wanunuzi wa ndani, ili kukuza bidhaa za Tanzania ziwe na ushindani zaidi katika soko la kimataifa."alisema.