Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

ZEEA, KUJA NA FURSA YA MASOKO ENDELEVU KWA WAJASIRIAMALI WA ZANZIBAR

  • August 6, 2024

01/8/2024
Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA) Ndugu Juma, Burhani Mohamed ametoa fursa kwa wajasiriamali wa Zanzibar kupitia mfumo wa masoko kidijitali unaowawezesha wajasiriamali kuuza bidhaa na huduma zao muda wowote na kokote dunia, ameyasema hayo katika mkutano wa ZEEA na waandishi wa habari kuelekea uzinduzi wa tamasha kubwa la biashara la Fahari ya Zanzibar ambapo TanTrade ni mbia ambaye anashirikiana na ZEEA katika kuandaa Tamasha na kuhakikisha fursa hizo za Masoko kwa wafanyabiashara zinapatikana