Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TAMASHA LA FAHARI YA ZANZIBAR LAVUMBUA FURSA ZA BIASHARA MKOA WA KASKAZINI

  • September 24, 2024

23 Septemba 2024

Tamasha la pili la Fahari ya Zanzibar lililoandaliwa na ZEEA pamoja Tantrade limeendelea kushika kasi kwakutoa elimu na kuvumbua fursa mbalimbali zikiwemo utalii, na mazao ya biashara, kama  vile karafuu nk, zilizopo Zanzibar ambapo leo imeendeshwa semina ya siku ya "Mkoa wa Kaskazini" ambapo mgeni rasmi ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Mgharibi Mhe Idrisa Kitwana ambaye anakaimu Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini, semina hiyo imefanyika katika Kiwanja cha Maonesho Nyamanzi Fumba tarehe 23 Septemba 2024.


 Mhe. Kitwana ametoa rai kwa wakazi wa mji huo kuendelea kufanya ubunifu wa miradi na biashara mbalimbali kwani serikali imekuwa ikitengeneza miundombinu na mazingira mazuri ya kibiashara katika mji huo hivyo kuwataka wakazi wa mkoa wa Kaskazini Unguja kuweza kujituma Katika utendaji kazi katika biashara zao.